.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 15 Julai 2015

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS ZANZIBAR, MAALIM SEIF ASEMA TANZANIA INAJIVUNIA HALI YA UTULIVU

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano la wafanyabiashara na wawekezaji mjini Milan Italia.

                                                                       (Picha na Salmin Said, OMKR Italy)

                        
                                                                                   Na: Khamis Haji, Italy

Makamu wa Kwanza wa Ras wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema Tanzania inajivunia hali ya utulivu wa kisiasa na hali ya kuwepo vivutio vingi vya uwekezaji vitega uchumi katika kuimarisha uchumi wake na kukuza maendeleo ya wananchi.


Akifungua Kongamano la Biashara katika maeneo ya biashara ya Kimataifa yanayofanyika Milan Italia, Maalim Seif ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa Italia na mataifa mengine kutumia fursa ya kuwepo mazingira hayo kufungua miradi ya uwekezaji nchini.

Alisema mbali na vivutio hivyo, Tanzania ipo katika eneo zuri na la kimkakati kibiashara kutokana na kuwa ni mlango mkuu wa kuingilia katika baadhi ya nchi jirani ambazo hazina bahari, zikiwemo Zambia, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Rwanda, Burundi na Malawi.

Maalim Seif aliwaeleza wajumbe wa kongamano hilo kutoka mataifa mbali mbali kuwa Tanzania inafuata misingi ya soko huria, ambayo wawekezaji na miradi yao ya vitegauchumi inapewa ulinzi kisheria chini ya Katiba ya nchi na sheria mbali mbali zinazohusu uwekezaji na biashara kimataifa.

Mapema Katibu Mkuu wa banda ya Italia katika maonesho hayo, Fabrizio Grillo akizungumza katika kongamano hilo alisema ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo unafungua milango zaidi ya uhusiano ya kiuchumi na kibiashara na ni fursa muhimu kati ya nchi mbili hizo.

Alisema Jumuiya ya Wafanyabiashara ya Milan imeandaa mazingira muafaka ya kufanikisha mawasiliano kati ya kampuni, serikali na wafanyabiashara mmoja mmoja kukaa na kufanya mazungumzo kwa azma ya kujuana na maeneo ambayo kila upande unavutika kuanzisha biashara.

Alisema maoneshi ya Milan 2015 ni ya kipekee kutokana na mikakati iliyoandaliwa kufanikisha biashara na uwekezaji na hadi sasa zaidi ya watu milioni sita wamejitokeza kwenye maonesho hayo.

Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo ni fursa ya kipekee kwa wawekezaji wa Italia kuchagua maeneo ya uwekezaji watakayoweza kuingia na kuzalisha kwa urahisi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni