Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dodoma
kwa tiketi ya CCM, Mariam Mfaki amefariki dunia leo mchana akiwa
amelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Mtoto wa marehemu Muhammed Mfaki
amesema mama yake alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani tangu
mwaka 2012.
Amesema kuwa mama yake Mariam hali
yake ilikuwa mbaya kuanzia juzi saa sita usiku na ndipo alipokimbizwa
katika hospitali ya mkoa wa Dodoma hadi umauti ulipomkuta hii leo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni