Mchezaji nyota mkongwe nchini Brazil
Pele ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji
uliofanikiwa wa mgongoni.
Pele mwenye umri wa miaka 74 alikuwa
akisumbuliwa na mishipa iliyojibana na alifanyiwa upasuaji ili
kumuondolea maumivu mgongoni na kwenye paja katika hospitali ya
Albert Einstein hospital Jijini Sao Paulo.
Pele, ambaye alitwaa kombe la dunia
mara tatu akiwa na timu ya taifa ya Brazil, miezi nane iliyopita
alitibiwa maambukizi katika mfumo wa haja ndogo pamoja na kuondolewa
mawe kwenye figo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni