.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 21 Julai 2015

GEORGE CLOONEY, AZINDUA MPANGO WA KUMALIZA TATIZO LA MIGOGORO HUKO SUDAN KUSINI

Mwigizaji wa kimataifa George Clooney, amezindua mpango maalum wenye lengo la kumaliza tatizo la migogoro huko Sudan Kusini na maeneo mengine Afrika, mkakati wake mkubwa ikiwa ni kufuatilia chanzo cha fedha zinazofadhili uhasama huo.

Akizindua mpango huo, Clooney mwenye umri wa miaka 54 sasa ameeleza kuwa, amani na haki halisi za binadamu zitasimama pale ambapo watu wanaofaidika kupitia vita watakapolipa uharibifu wanaosababisha.

Kati ya shughuli ambazo zitafanyika kupitia mpango huu, ni uchunguzi wa wafadhili wanaowezesha kuendelea kwa machafuko ya mara kwa mara katika maeneo ya Afrika ya Kati ikiwepo Sudan na vilevile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni