Vituo vya kupigia kura nchini
Burundi vimefunguliwa leo tangu majira ya kumi na mbili asubuhi,
baada ya jana usiku kusikika milio ya risasi na milipuko katika Jiji
la Bujumbura.
Rais Pierre Nkurunziza anawania
urais kwa muhula wa tatu mfululizo katika uchaguzi huo ambao
umepingwa na wapinzania kutokana na kukiuka Katiba.
Wananchi wamechukizwa na hatua ya
rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu na kuibua machafuko tangu
Aprili mwaka huu na kufuatiwa na jaribio la mapinduzi mwezi Mei,
mwaka huu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni