Mke wa muigizaji filamu Johnny Depp,
Amber Heard sasa ameshafunguliwa mashtaka ya kuingiza mbwa kimagendo
nchini Australia.
Heard ambaye naye ni muigizaji
filamu alijikuta matatani kwa kuingia bila ya taarifa na mbwa wawili, wakati akiwa anawasili huko Brisbane mwezi Aprili.
Heard sasa amefunguliwa mashtaka
mawili ya kuingiza kinyume na sheria mbwa hao pamoja na kutoa nyaraka
za uongo.
Iwapo atatiwa hatiani kwa kosa hilo
atakabiliwa na faini kubwa ama kifungo jela cha zaidi ya miaka 10.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni