Mtu mwenye silaha amewaua kwa
kuwapiga risasi wanajeshi wanne wa Marekani na kuwajeruhi wengine
kadhaa katika majengo mawili ya Kikosi cha Jeshi cha Majini cha
Marekani huko Chattanooga, Tennessee.
Mwanasheria wa wilaya amesema
matukio hayo ya mashambulizi ya kutumia risasi yanachunguzwa na
kusema kuwa kitendo hicho ni tukio la ugaidi wa ndani ya nchi.
Mtu huyo mwenye silaha alipigwa
risasi na kufa ametambuliwa kuwa ni kijana wa miaka 24 Mohammad
Youssuf Abdulazeez mzaliwa wa mashariki ya kati.
Rais Barack Obama amesema shambulio
hilo ni la kuvunja moyo, na kuongeza kuwa mtuhumiwa alitekeleza
uhalifu huo akiwa peke yake.
Mtuhumiwa Mohammad mwenye fulana ya rangi ya chungwa akiwa na familia yake.
Kikosi cha S.W.A. T. kikifanya ukaguzi katika eneo la tukio
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni