Jaji wa mahakama amepunguza kiasi
cha dola milioni 1, kutoka katika kiasi cha fidia aliyopaswa kulipa
Pharrell Williams, kutokana na wimbo wake wa Blurred kuvunja sheria
ya hati miliki.
Kesi hiyo ilihusu iwapo Williams na
mwandishi mwenzake wa mashairi ya wimbo huo Robin Thicke walinakili
kazi ya Marvin Gaye ya mwaka 1977 ya kibao chake cha Got To Give It
Up.
Mwezi Machi, jopo la mahakama
liliridhia familia ya Gaye kulipwa fidia ya dola milioni 7.3, lakini
sasa Jaji wa mahakama ya Wilaya John A Kronstadt amepunguza fidia
hiyo kuwa dola milioni 5.3.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni