Wazazi wa Teso Kaskazini nchini
Kenya wamepigwa na butwaa kufuatia miguu ya watoto wao kuishiwa nguvu
na kupooza baada ya kuchomwa sindano katika Zahanati.
Wakazi hao jana walilazimika kuvamia
ofisi ya Gavana Sospeter Ojaamong, wakiwatuhumu wafanyakazi wa
Zahanati ya Akichelesit kwa kuwadhuru watoto wao.
Karibu familia 30, zimesema watoto
wao wamedhurika na ugonjwa wa ajabu baada ya kuchomwa sindano katika
Zahanati hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni