Mwandishi mkongwe wa habari nchini Said Kubenea ametangaza rasmi nia yake ya kutaka kuwania ubunge katika jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema ).
Kubenea ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mwanahalisi Publishers ametangaza nia hiyo mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za makao makuu ya Chadema zilizopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Mbunge wa Ubungo hivi sasa ni Mh John Mnyika ambaye pia ni mwanachama wa Chadema.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni