Imeelezwa kuwa panya ndiye aliyekuwa
chanzo cha tukio la waumini wanawake kukanyagana kwenye msikiti mmoja
katika mji wa Casablanca nchini Morocco na kusababisha watu 80
kujeruhiwa.
Maafisa wa nchi hiyo wamesema
waumini waliokua msikitini walizimia baada ya panya kukatiza kwenye
mguu wa mwanamke mmoja aliyekuwa anaswali, na kulazimika kukimbia nje
na kusababisha hofu kwa wengine.
Tukio hilo la kukimbia na
kukanyagana katika msikiti wa Hassan II, lilitokea jumatatu usiku
wakati waumini wakiendelea na swala katika kipindi hiki cha mfungo wa
mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni