Hatimae Mbunge wa Jimbo la Mbeya
mjini, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mh. Joseph Mbilinyi almaarufu Sugu amepata mpinzani aliyetangaza nia
leo ya kuwania kiti hicho ndani ya Chama hicho.
Akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari mara baada ya kuchukuwa fomu ya Ubunge katika
Ofisi za chama hicho Wilaya ya Mbeya mjini,Mwandishi wa habari
Mkongwe na mwakilishi wa kampuni ya magazeti ya Free Media mkoani
mbeya,Christopher Nyenyembe amesema endapo atapata ridhaa ya
kupeperusha bendera ya Chadema atakuwa jirani na wananchi kusikiliza
vipaumbele na kuahidi kuvitekeleza kwa asilimia 100.
Bw. Nyenyembe ambaye amewahi kuwania
nafasi ya Ubunge jimbo la Mbeya mjini katika uchaguzi mkuu mwaka 2010
na kushika nafasi ya tatu kwa tiketi ya Chadema akitanguliwa na
Mh.Sugu na kufuatiwa na Mponzi ametaja kipaumbele cha pili ni
kuwasemea wanahabari wote mkoani Mbeya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni