Swala ya maziko ya watu wengi
imefanyika nchini Uturuki kwa wanaharakati 32 waliouwawa katika tukio
la bomu la kujitoa mhanga huko Suruc, karibu na mpaka wa Syria.
Waombolezaji waliotiririkwa na
machozi walionekana wakipaza sauti zao huku wakiwa wamebeba majeneza
yenye miili ya wanaharakati hao katika eneo la msikiti.
Waziri Mkuu wa Uturuki amesema
mamlaka imembaini mtuhumiwa wa mlipuko huo, ambaye inadhaniwa kuwa na
ushirikiano na kundi la Dola ya Kiislam (IS).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni