Aliyekuwa rais wa Marekani, Jimmy
Carter amesema upasuaji wa ini aliofanyiwa hivi karibuni umebaini
kuwa anaugua saratani na imesambaa kwenye sehemu nyingine za mwili
wake.
Carter mwenye umri wa miaka 90,
alifanyiwa upasuaji wa kuondolewa viuvimbe vidogo kwenye ini lake
mapema mwezi huu.
Rais huyo wa zamani wa Marekani
aliyeondoka madarakani mnamo mwaka 1981, amesema kuwa atabainisha
zaidi matatizo yanayomkabili baada ya kupata uhakika ifikapo wiki
ijayo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni