Mlipuko mkubwa uliotokea katika mji
wa Tianjin kaskazini mwa China umeuwa watu 50 huku wengine wapatao
700 wakijeruhiwa.
Chombo cha habari cha serikali
kimesema mlipuko huo umetokea kwenye ghala lililokuwa limehifadhia
kemikali hatari katika bandari ya mji huo, ambapo miongoni waliokufa
wapo askari 12 wa zima moto wengini 36 hawajulikani walipo.
Picha na video kwenye mitandao ya
jamii zimnaonyesha moto mkubwa ukitanga angani, na kunamajengo
yameripotiwa kuanguka. Taarifa zinaeleza hospitali zimezidiwa na
majeruhi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni