Kiongozi wa chama cha upinzani cha
CORD, Raila Odinga amemkosoa rais Uhuru Kenyatta kwa kutia saini
makubaliano ya uagizaji sukari kutoka Uganda, na kutahadharisha kuwa
yatauwa kabisa viwanda vya ndani vya sukari.
Raila pia amehoji makubaliano ya
Kenya kusafirisha nyama pamoja na mazao ya maziwa nchini Uganda, kwa
kusema kuwa mazao hayo mawili hayatoshelezi soko la ndani la Kenya
kwa sasa iweje yasafirishwe nje ya nchi.
Katika kuonyesha upinzani kuponda
makubaliano hayo ya kibiashara baina ya nchi za Kenya na Uganda,
Odinga amesema kuwa masilahi binafsi ya biashara ndio yamewekwa mbele
badala ya maslahi ya taifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni