Serikali ya Mexico imepiga marufuku
utoaji wa maziwa ya kopo ya bure kwa watoto wachanga hospitalini ili
kuhamasisha wakina mama kunyonyesha watoto maziwa ya mama.
Wizata ya Afya ya nchi hiyo imesema
kuanzia sasa maziwa ya watoto ya kopo yatapatikana kwenye maduka na
yatanunuliwa pale tu ambapo kutakuwa na maelezo ya daktari.
Serikali imesema inataka kuhamasisha
unyonyeshaji maziwa ya mama, ambapo takwimu zinaonyesha Mexico ina
kiwango kidogo mno cha unyonyeshaji katika mataifa ya Latini Amerika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni