Mlipuko katika soko lenye watu wengi
kaskazini-mashariki mwa Borno nchini Nigeria umeuwa watu wapatao 47.
Watu zaidi ya 52 wanaaminika kuwa
wamejeruhiwa, chanzo kutoka jeshi la Nigeria kimelieleza shirika la
habari la Reuters.
Mlipuko huo umetokea katika soko la
wanyama katika mji wa Sabon Gari kusini mwa Borno, majira ya saa saba
na nusu. Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wameua mamia ya watu
katika jimbo hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni