Asali ikiwa imechanganywa na mdalasini tayari kwa matumizi
|
ASALI na MDALASINI zinasaidia kuponyesha kwasababu zina tabia za ANTI-BACTERIAL( zinaua na kuzuia mazalia ya bacteria)
Jinsi ya kufanya:-
1. Chukua vijiko vitatu(3) vya chai vya ASALI
2. Chukua nusu kijiko cha chai cha MDALASINI WA UNGA safi
3. Changanya pamoja kupata uji uji mzuri
4. Paka sehemu yenye chunusi na kisha kaa nayo kwa angalau dakika 10-30 kisha osha kwa maji ya uvuguvugu.
ANGALIZO: MDALASINI unaweza kuwasha kwenye ngozi hivyo unashauriwa ujaribu kupaka kidogo kwenye kiganja cha mkono kwanza ili kupata uhakika kua haitakusumbua.
(Imeandaliwa na Honey Spring na Jamiimojablog)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni