|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
|
Mke
wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete akizungumza na umati wa wanaCCM na
wapenzi wa chama hicho uliokuwa umefurika katika uwanja wa Mnazi Mmoja
nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea
mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu.
|
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM pamoja na wananchi viwanja vya Mnazi Mmoja. |
|
|
|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Katibu,
Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na wanaCCM na
wananchi kwenye mkutano wa kampeni za mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia
Suluhu jana Mkoani Lindi. |
|
Bi.
Samia Suluhu (kulia) akimtambulisha mgombea mmoja wa wagombea udiwani
katika Jimbo la Mchinga, kuzungumza na wapiga kura wa eneo hilo. |
|
Samia Suluhu akimpokea mmoja wa wanachama mpya aliyejiunga na CCM katika Jimbo la Mchinga. |
|
Bi. Samia Suluhu akimpokea mmoja wa wanachama mpya aliyejiunga na CCM katika Jimbo la Mchinga.
|
|
Mmoja wa wanachama wapya wa CCM aliyejiunga na CCM mara baada ya mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza katika Jimbo la Mchinga. |
KAMPENI za mgombea mwenza wa
nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia Suluhu
zinazoendelea mkoani Lindi zimekuwa tishio kwa vyama vya upinzani baada
ya mkutano uliofanyika jana eneo la Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa
Lindi Mjini kuzoa wanachama 61 waliotoka upinzania na kujiunga na CCM.
Mkutano huo wa kampeni uliohudhuriwa pia
na Mke wa Rais Mama Salima Kikwete umeacha maumivu kwa vyama vya
upinzani vya CUF, Chadema na NCCR-Mageuzi baada ya kujikuta wanachama 61
wakivikimbia vyama vyao na kujikuta wakijiunga na Chama Cha Mapinduzi
na kukabidhiwa kadi mpya za CCM kila mmoja.
Miongoni mwa wanachama ambao
walipokelewa leo ni pamoja na Katibu wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini,
Abdullah Madebe, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi Mtaa wa Nananji Lindi,
Bakari Kalulu na wanachama wengine kutoka vyama vya CUF na Chadema.
Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi, Bi. Samia Suluhu Katibu wa Chadema
Wilaya ya Lindi Mjini alisema awali alipokuwa upinzani alikuwa amepotea
na amegunduwa kuwa alikuwa anapoteza muda hivyo kuomba wananchi
wamsamehe na ameamua kurudi kundini na kuendelea kulkijenga taifa.
Akizungumza baada ya kuwapokea wanachama
hao, mgombea mwenza Suluhu alisema Serikali ya awamu ya tano imeandaa
mambo mengi mazuri kwa mikoa ya Lindi na Mtwara na jambo la kwanza
kulifanya baada ya kuunda serikali ni kuubadili mji wa Mtwara na Lindi
kuwa miji ya viwanda, hali ambalo itakuza uchumi kwa kiasi kikubwa hivyo
kunufaisa wananchi.
Alisema kwa kuanzia Serikali inajenga
viwanda vinane mkoani Mtwara na vingine vitajengwa mkoani Lindi viwanda
ambavyo vitategemea gesi katika uzalishaji wake bidhaa ambayo tayari
inapatikana kwa wingi katika maeneo hayo. Alisema ujenzi wa viwanda
utaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuongeza nafasi za ajira jambo
ambalo litawanufaisha wakazi wa eneo hilo na wawekezaji.
"...Tunataka kuitenga Lindi kuwa mji wa
viwanda vitakavyoitumia gesi kwa uendeshaji, lengo ni kuwa na viwanda
vitakavyozalisha nafasi za ajira takribani asailimia 40...," alisema Bi.
Suluhu. Awali akihutubiwa katika mkutano wa kampeni ulofanyika Kata ya
Mingumbi Kilwa Kusini, alisema Serikali inatambua hali ya kuyumba kwa
soko la korosho na ufuta ili kukabiliana na hali hiyo imejipanga kujenga
viwanda vya kubangua na kufunga korosho pamoja na kukamua mafuta kwa
lengo la kumuongezea thamani mkulima katika zao analozalisha.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa
Mnazi Mmoja Katibu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye aliwatoa hofu
akinamama na wapiga kura wengine juu ya vitisho vya kuwepo na vurugu
kipindi cha uchaguzi kwa lengo la kuwatisha wapiga kura, hivyo kuwataka
wananchi wasiogope kwani Serikali na CCM kupitia vijana wake imejipanga
kupambana na wafanya fujo hao.
Alisema kitendo cha kutoa vitisho kwa
wapiga kura ni kuibaka demokrasia hivyo CCM na vijana wake hawatakuwa
tayari kuona demokrasia inabakwa nchini na wapuuzi wachahe. "...Vijana
wa CCM naomba mkikamata kibaka wa demokrasia shughulikeni naye kidogo
kabla ya kumpeleka polisi...CCM itashinda kwa kishindo," alisema Nape
Nnauye.
Aidha msemaji huyo wa Chama Cha
Mapinduzi alisema mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa pamoja na
mpambe wake anayemuunga mkono Fredrick Sumaye hawawezi kuiponda Serikali
ya CCM kwa kuwa wao wamekuwemo na kushika nafasi za juu za utendaji
ndani ya serikali na kama walishindwa kuleta mabadiliko hawawezi kufanya
hivyo leo.
Aliongeza kuwa kitendo cha kuendelea
kuiponda ni sawa na kujidhalilisha wao wenyewe kwa wananchi hivyo
kuwataka wasiwarubuni Watanzania kwamba wanamabadiliko ya msingi zaidi
ya maslahi yao binafsi, ambayo ndiyo yanayowasukuma kukimbilia walipo.
Mgombea mwenza wa urais CCM, Bi. Suluhu
bado anaendelea na ziara ya kuinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Mkoani
Lindi na baada ya kumaliza majimbo ya mkoa huo ataendelea katika Mkoa wa
Mtwara, kuwashawishi wananchi kuichangua CCM ili iweze kupata ridhaa ya
kuunda Serikali ya awamu ya tano.
|
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Suluhu kwenye Jimbo la |
|
Kutoka
kushoto ni mgombea mwenza wa CCM nafasi ya uraisa, Bi. Samia Suluhu na
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Maiza na mgombea wa Jimbo la Mchinga
Said Mtanda wakiwa kwenye mkutano wa kampeni katika Jimbo la Mchinga
jana. |
|
Mgombea
Jimbo la Mchinga Said Mtanda akizungumza na wannaCCM na wananchi jana
jimboni kwake ambapo mgombea mwenza alihutubia wananchi. |
|
Sehemu ya wanaCCM na wananchi jana jimboni kwake ambapo mgombea mwenza alihutubia wananchi. |
|
Mbunge
wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Anjela
Kiziga akizungumza katika mkutano wa kampeni za CCM. |
|
Aliyekuwa
Mjumbe wa Kamati ya Ushindi Chadema Taifa, Greison Nyakarungu ambaye
kwa sasa amejiunga na CCM akizungumza katika moja ya mikutano ya kampeni
ya CCM. |
|
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumpta Mshama akipiga madongo kwa wapinzani kwenye moja ya mikutano ya kampeni ya CCM. |
|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Katibu, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bi. Mwantumu Mahiza. |
|
Umati
wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika uwanja wa
Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa kampeni
wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza akizungumza na wanaCCM na wananchi
kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM, Mama Samia Suluhu. |
|
Mke
wa Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi,
Mzee Ally Mtopa pamoja na mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi.
Samia Suluhu wakijadiliana jambo kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea
mwenza wa CCM viwanja vya Mnazi Mmoja. |
|
Sehemu
ya umati wa wanaCCM na wapenzi wa chama hicho ukiwa umefurika katika
uwanja wa Mnazi Mmoja nje kidogo ya mji wa Lindi Mjini kwenye mkutano wa
kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi, Bi. Samia Suluhu. |
|
Katibu
wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini, Abdullah Madebe akikabidhi kadi ya
chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). |
|
Aliyekuwa
Katibu wa Chadema Wilaya ya Lindi Mjini, Abdullah Madebe (kulia)
akipongezwa na Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu
mara baada ya kujiunga na CCM, Katikati ni Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete. |
|
Mmoja wa wananchi waliojiunga na CCM katika mkutano huo akizungumza baada ya kujiunga na chama hicho tawala. |
|
Mmoja wa wananchi waliojiunga na CCM katika mkutano huo akizungumza baada ya kujiunga na chama hicho tawala. |
|
Mama Salma Kikwete pamoja na Bi. Samia Suluhu wakipokea kadi za wanachama waliojiunga na CCM jana Mkoani Lindi. |
|
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Mzee Ally Mtopa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa CCM viwanja vya Mnazi Mmoja. |
|
Kada
wa CCM na mbunge wa zamani wa Mchinga, Mudhir Mudhir akizungumza na
wanaCCM pamoja na wananchi wa Jimbo la Mchinga katika mkutano wa
kampeni. |
*Imeandaliwa/www.thehabari.com
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni