.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 14 Septemba 2015

BALOZI SEIF AZINDUA MASKANI YA VIJANA WA CCM WA JIMBO KIWANI

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif akizindua Maskani ya CCM ya Vijana wa Jimbo la Kiwani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba iliyopewa jina lake.
Balozi Seif akipandisha Bendera ya Maskani ya CCM ya Vijana wa Kiwani Iliyopewa jina la Balozi Seif Maskani mara baada ya kuizindua rasmi katika sherehe iliyofanyika Jimboni humo.
Baadhi ya wanachama wa CCM na Wsananchi wa Kijiji cha Kiwani Michakweni wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif hayupo Pichani wakati wa uzinduzi wa Maskani ya Jina wa Kijiji hicho iliyopewa jina lake.
Balozi Seif akisalimiana na Sheikh Faki Mohammed Khamis ambae ni mlemavu asiyeona baada ya kusoma Quran Tukufu wakati wa uzinduzi wa Balozi Seif Maskani hapo Kiwani Wilaya ya Mkoani.
Vijana wa Maskani ya CCM ya Balozi Seif iliyopo Kiwani wakitoa burdani ya nyimbo maalum iliyoanikiza katika uzinduzi wa Maskani yao waliyoamua kuipa jina la Balozi Seif Maskani.
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwakumbusha Vijana wa Kiwani Michakweni kuelewa wajibu wao wa kuhakikisha CCM Inaendelea kushika dola kwa kuwapa ushindi wagombea wa Chama hicho.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Kiwani mara baada ya kuizindua Balozi Seif Maskani ya Kijiji hicho.
Haiba ya Jengo la Balozi Seif Maskani liliopo Kiwani Kichakweni lililojengwa kwa kuzingatia Utamaduni wa Visiwa vya Zanzibar. Picha na – OMR – ZNZ

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha
Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi amewaasa Wanachama wa Vyama vya
upinzani Kisiwani Pemba kuacha kuendelea kukumbatia Viongozi ambao
tayari wameshaonyesha muelekeo wa kutokubali kusimamia maendeleo yao
kwa zaidi ya miaka Ishirini sasa.
Alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na Wanachama wa Chama cha
Mapinduzi { CCM } na Wananchi wa Kijiji cha Kiwani – Michakweni Jimbo
la Kiwani mara baada ya kuizindua Rasmi Maskani ya Vijana wa CCM wa
Jimbo hilo iliyopewa Jina lake.
Balozi Seif alisema wakati wa kuacha kudanganywa kwa sera na ahadi
zisizotekelezeka za Viongozi hao wanaojali maslahi yao binafsi umefika
kwa wafuasi hao wa Upinzani na badala yake wajiunge na Chama cha
Mainduzi kabla hawajaachwa njia panda.
Alisema Gari la Chama cha Mapinduzi hivi sasa bado linaruhusu
kupakiwa abiria wowote watakaoamua kutoka vyama vya upinzani ambao
wanaonekana kuchoshwa na vitendo vinavyoviza Maendeleo yao kwa kiindi
kirefu sasa.
Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na Wananchi walio wengi
Kisiwani Pemba kuonyesha dalili za kuchoshwa na hatimae kukataa
Viongozi wasiojali Maendeleo ya Wananchi.
Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alisema katika kuuzika upinzani
katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mfumo wa Vyama vingi vya Siasa
aliwakumbusha Wana CCM waendelee kushikamana lengo likiwa ni kumaliza
upinzani huo usio na muelekeo wa Maendeleo.
Amewapongeza Vijana hao wa Balozi Seif Maskani wa Kiwani Michakweni
kwa uamuzi wao wa kujenga Jengo lililozingatia Utamaduni wao na
kuwaahidi kusaidia kuiimarisha katika kiwango kinacholingana na Chama
chenyewe.
Alisema msaada huo utakwenda sambamba na kuzingatia mipango imara ya
kuwapatia Boti ya uvuvi itakayowapa fursa ya kujiajiri wenyewe ili
waweze kukidhi mahitaji yao ya Kimaisha.
Balozi Seif alieleza kwamba tabia ya kukaa vijiweni hivi sasa imepitwa
na wakati kulingana na mabadiliko ya mfumo wa Dunia uliopo hivi sasa
ambao unamkaba mwanaadamu lazima afanye kazi.
Akitoa Taarifa fupi ya Vijana hao wa Balozi Seif Maskani Mmmoja wa
Viongozi wa Maskani hiyo Ndugu Mohammed Juma alisema Maskani hiyo
imeasisiwa Mwaka 2014 ikianza na Wanachama 22 na hivi sasa imeongeza
wanachama na kufikia 36.
Nd. Mohammed alisema kwamba Vijana hao wamejipanga kuwa Maskani ya
chuo cha Vijana katika kuwafundisha sera za Chama cha Mapinduzi
pamoja na Itikadi zake zitakazosaidia Vijana hao kuelewa Historia ya
Taifa hili lililojikomboa kutokana na madhila ya wakoloni.
Vijana hao wa Balozi Seif Maskani Kiwani Michakweni wameupongeza
Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mkoani kwa kuwahakikishia usalama
licha ya vitisho wanavyoendelea kufanyiwa na wafuasi wa Upinzani kwa
uamuzi wao wa kuunga mkono Chama cha Mapinduzi.
Naye akisalimia na Vijana hao wa Balozi Seif Maskani ya Kiwanchi
Michakweni Mke wa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mama Asha
Suleiman Iddi amewataka akina Mama wa Kijiji na Jimbo hilo kuhakikisha
kwamba Viongozi watakaowachaguwa wawe tayari kufanya nao kazi pamoja.
Mama Asha alisema wapo viongozi wenye tabia ya kwenda Majimboni
kuomba kura na baadaye kuwatelekeza Wananchi hao bila ya kujali kwa
vitendo vyao vya kutafuta maslahi katika maeneo mengine vinawanyima
haki Wananchi wao.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni