.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 13 Septemba 2015

MGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR, MAALIM SEIF AUNGURUMA JIMBO LA MFENESINI

Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wafuasi wa chama hicho katika viwanja vya Mwakaje Jimbo la Mfenesini.
                                                                              Baadhi ya wafuasi wa chama hicho

                                                                            Na: Hassan Hamad (OMKR)

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewatoa hofu wananchi wenye asili ya Tanzania Bara kuwa wataendelea kuishi Zanzibar kwa usalama bila ya usumbufu wa aina yoyote.

Amesema maneno yanayoenezwa na baadhi ya vyama vya siasa kuwa iwapo watamchagua Maalim Seif kuwa Rais atawafukuza Zanzibar, ni propaganda zisizokuwa za kweli wowote.

Akizungumza na wafuasi na wapenzi wa chama hicho kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mwakaje jimbo la Mfeneseni, Maalim Seif amesema hana historia ya kuwabagua watanzania bali kuwaunganisha, na kwamba umoja ndio utakaleta maendeleo ya haraka nchini.

“Nimekuwa kiongozi wa kitaifa kwa muda mrefu na hivi sasa mimi ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, mulishawahi kusikia kuwa nimembagua mtu”, alihoji Maalim Seif.

Kuhusu sekta za maendeleo, Maalim Seif amesema anakusudia kuimarisha sekta za kilimo, mifugo na uvuvi ambazo ndizo zinazotoa ajira nyingi kwa wananchi wa Zanzibar.

Amesema atahakikisha kuwa pembejeo za kilimo, vifaa vya uvuvi na mifugo ya kisasa inapatikana, ili kuwawezesha wananchi kuongeza kipato chao.

Kwenye sekta ya afya, Maalim Seif ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema atashirikiana na washirika wa maendeleo ili kuweka udhibiti wa madawa kuanzia hatua ya kuingizwa bohari kuu hadi kumfikia mgonjwa, kwa lengo la kuepusha upotevu wa madawa wanayonunuliwa na serikali.

Amesema Hospitali kuu ya Mnazimmoja itapatiwa vitendea kazi vyote muhimu katika kipindi kifupi cha uongozi wake vikiwemo wataamu na vifaa, ili kuipa hadhi ya hospitali hiyo kuwa ya rufaa kivitendo.

Aidha amesema ataendeleza sekta ya utalii kwa kuwahamasisha watalii wa daraja la juu wataoweza kutumia fedha nyingi na kusaidia kunyanyua uchumi wa Zanzibar.

Amefahamisha kuwa ataweka mazingira ya kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inawanufaisha wazawa, na sio nafasi zote kuchukuliwa na wageni hata zile nafasi ambazo wazanzibari wana ujuzi nazo.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amewataka wanachama hao kudhibiti shahada zao za kupigia na wasikubali kurubuniwa kuuza shahada hizo.

“Wanaweza kuja watu wakataka muwape shahada zenu za kupigia kura, nakunasihini hata kuwaonesha musiwaoneshe achilia mbali kuwapa. 

Mujue kuwa mukizitoa shahada zena itakuwa mumeuza utu wenu kwa kipindi cha miaka mitano ijayo”, alinasihi Mazrui.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni