Hatua ya kujihusisha kijeshi nchi ya
Urusi katika nchi ya Syria inatarajiwa kuwa ni moja ya agenda kuu
wakati mawaziri wa ulinzi wa Nato wanapokutana Jijini Brussels nchini
Ubelgiji.
Mkutano huo umeitishwa baada ya
Uturuki ambayo ni mjumbe wa Nato kulalamika kuwa ndege za Urusi
zimekuwa zikikiuka sheria mara kwa mara kwa kukatiza katika anga
yake.
Urusi imekuwa ikilalamikiwa kwa
kuwashambulia pia waasi wa Syria wanaoungwa mkono na Marekani na
washirika wake badala ya kuwashambulia wapiganaji wa Dola ya Kiislam
(IS).
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni