Watu 13 wameripotiwa kuuwawa kwa
mashambulizi ya anga yaliyolenga harusi katika eneo linaloshikiliwa
na waaasi nchini Yemen.
Kwa mujibu wa mashuhuda shambulio
hilo limetokea eneo la Sanban kilomita 100 kusini mashariki mwa Jiji
Kuu la Sanaa.
Haikufahamika wazi nani haswa
anahusika na shambulio hilo, ingawa vikosi vinavyoongozwa na Saudi
Arabia vimekuwa vikifanya mashambulizi ya anga dhidi ya waasi wa
Houthi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni