Mwanaume wa miaka 27 amemchoma visu
mpenzi wake na kumuua na baadae naye kujiuwa kwa kunywa sumu katika
makazi ya Juja B Jijini Nairobi nchini Kenya.
Mkuu wa kituo cha polisi cha
Starehe, Benard Nyakwaka, amesema ugomvi huo baina ya wapenzi hao
wawili umetokea saa saba na dakika arubani usiku wa kuamkia leo.
Mwanaume huyo Abdi Malik Idris,
amemchoma visu mara saba Santa Mohamed Abdullah katika ugomvi huo wa
mapenzi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni