Mlipuko wa ugonjwa ujulikanao kama
mafua ya nguruwe katika eneo la kusini mashariki mwa Iran umeuwa watu
33 katika wiki tatu zilizopita.
Naibu Waziri wa Afya wa Iran,
Ali-Akbar Sayyari ameliambia shirika la habari la IRNA watu 28
wamekufa katika mkoa wa Kerman na wengine watano huko
Sistan-Baluchistan.
Waziri Sayyari ameonya kuwa mlipuko
huo wa mafua ya nguruwe unaosambazwa na virusi vua H1N1 unaweza
kusambaa maeneo mengine ya Iran ikiwemo Jiji la Tehran.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni