Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius anatarajiwa kufika mahakamani kuomba dhamana baada ya jaji
kubadilisha hukumu yake ya kuuwa bila ya kukusudia na kuwa kesi ya
mauaji ya kukusudia wiki iliyopita.
Mwanariadha huyo mlemavu sasa
anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela kwa kumuua mpenzi wake Reeva
Steenkamp mwaka 2013.
Pistorius alimuua Reeva Steenkamp
siku ya wapendanao kwa kumpiga risasi nne zilizopenya kwenye mlango
wa choo uliofungwa na kumpata.
Kwa sasa Pistorius alikuwa
anatumikia kifungo cha nyumbani baada ya kukaa jela kwa mwaka mmoja
katika adabu ya kifungo cha mwanzo cha miaka mitano.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni