Mwanaume mmoja mwenye kisu amemkata
mtu mmoja Jijini London kwenye kituo cha treni ya aridhini, huku
akisema anafanya hivyo kwa ajili ya Syria, hata hivyo baadae
alidhibitiwa na polisi kwa kutumia siala za shoti ya umeme.
Tukio hilo limeelezwa na kikosi cha
Scotland Yard kama ni tukio la ugaidi, na mashuhuda wameeleza mtu
huyo alisikika akisema anafanya hivyo kwa ajili ya kulipiza
mashambulizi ya anga yanayofanyika Syria na atahakikisha damu za watu
wengi zinamwagika.
Wakati wa tukio hilo watoto
waliojawa na hofu walikimbia huku wazazi wao waliokatwa kwa visu
wakianguka sakafuni huku tiketi zao zikiwa zimetapakaa damu.
Mti aliyekatwa kwa kisu akiwa sakafuni huku damu zikimtoka
Polisi akitumia silaha ya shoti ya umeme kumdhibiti mtu mwenye kisu
Mtu mwenye kisu akiwa chini baada ya kupigwa shoti
Polisi wakimdhibiti mtu aliyekuwa na kisu kwa kumfunga mikono pingu kwa nyuma
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni