Mmoja wa polisi aliyeshiriki katika
kudhibiti tukio la mashambulizi katika eneo la mikusanyiko kwa ajili
ya sherehe za kijamii Jijini California nchini Marekani ameelezea
hali aliyoikuta ilikuwa haielezeki.
Polisi huyo Luteni Mike Madden
amesema yeye pamoja na maafisa wengine walipofika katika tukio hilo
walikuta miili ya watu waliokufa na waliwapita watu waliojeruhiwa
wakati wakikabiliana na wavamizi wenye silaha waliouwa watu 14 na
kuwajeruhi 24.
Luteni Madden amesema kuwa watu hao
ambao ni mtu na mkewe waliwafyatulia risasi na kuwauwa watu 14 na
kuwajeruhi wengine 21 katika mji wa San Bernardino siku ya jumatano. Washambuliaji hao Syed Rizwan
Farook, 28, na Tashfeen Malik, 27, nao wameuwawa katika tukio hilo.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni