Rais wa Nigeria ametangaza mipango
ya kuongeza matumizi ya serikali yake kwa asilimia 20 mwakani, kwa
kukopo mno kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta.
Katika bajeti yake ya kwanza tangu
ashinde uchaguzi mwezi Machi, Muhammadu Buhari amesema atatumia dola
bilioni 31 mwaka 2016 katika miundombinu na uchumi.
Hata hivyo Nigeria inakabiliwa na
tatizo la kushuka kwa bei ya mafuta, ambapo mauzo ya petroli
yanaiingizia nchi hiyo asilimia 90 ya pato lake la nje.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni