Shule Jijini Beijing zitafungwa na
kazi za ujenzi wa nje kusimamishwa baada ya Jiji hilo la China kutoa
tahadhari ya alama nyekundu ya uchafuzi wa hewa uliosababisha ukungu
wa moshi.
Tahadhari ya alama nyekundu ya
uchafuzi wa hewa ni ya juu mno na haijawahi kutolewa katika Jiji hilo
katika miaka ya nyuma, kwa mujibu wa shirika la habari la China la
Xinhua.
Mamlaka za Jiji la Neijing
zinatarajia kuwepo kwa ukungu huo wa moshi kwa siku tatu mfululizo,
ambapo magari yenye namba za zamani yatazuiwa kutembea katika siku
hizo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni