Bendi ya muziki wa Rock ya U2
imeandika wimbo maaluma kwa ajili ya watu wa Paris baada ya kutokea
mashambulizi ya kigaidi yaliyouwa watu 130.
Kundi hilo lilikuwa lifanye tamasha
lake katika Jiji hilo la Ufaransa siku kadhaa baada ya mashambulizi
hayo lakini ilibidi lihairishe.
Wakati wakiimba wimbo huo jana Paris
Bono alijifunika bendera ya Ufaransa akiimba mashairi ya muimbaji wa
Ufaransa Jacques Brel ya "Ne me quitte pas," kwa lugha ya
Kingereza "Don't Leave Me".
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni