Wanaume wawili wa Burma wametiwa
hatiani na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kuhusika na mauaji ya
watalii wawili raia wa Uingereza, mwaka jana.
Jaji amesema watuhumiwa hao Zaw Lin
na Wai Phyo waliwauwa Hannah Witheridge, 23, anayetokea Norfolk
pamoja na David Miller, 24, anayetokea Jersey.
Miili ya raia hao wa Uingereza
ilipatikana kwenye fukwe ya kisiwa cha Koh Tao Septemba mwaka 2014.
Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao wamesema watakata rufaa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni