Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akiingia katika ukumbi wa mikutano katika kitengo cha Moyo cha Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete kilichopo katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili, ambapo amepongeza weledi wa huduma za madaktari na wauguzi kutokana na huduma zinazotolewa katika Tasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu akimkaribisha Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ili aweze kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kupongeza jopo la Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili.
Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kupongeza jopo la Madaktari waliomhudumia katika Hospitali ya Mhimbili kutoka kushoto ni Profesa Mohamed Janabi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo na Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Dkt. Mpoki Ulisubisya na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu
Profesa Mohamed Janabi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo akimshukuru Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kwa kutoa zawadi za kadi za pongezi kwa baadhi ya madaktari na wauguzi wa Taasisi hiyo ya moyo kushoto ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu
Profesa Mohamed Janabi Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete akiwafafanulia waandishi wa habari mambo mbalimbali waliyotaka kujua kuhusu taasisi hiyo katikati ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee Mhe Ummy Mwalimu na kushoto ni Katibu Mkuu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, watoto na Wazee, Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni