Baraza la Marekani la Dini ya
Kiislam, limemtaka muwania urais kwa tiketi ya Republican Donald
Trump kuomba msamaha kwa mfuasi wa dini ya Kiislam aliyeondolewa
kwenye mkutano wake.
Baraza hilo, limesema kitendo cha
kuondolewa mkutanoni kwa muumini huyo wa Kiislam Bi.
Rose Hamid, huko Carolina ya Kusini,
kinatoa picha mbaya kwa jamii ya Waisalam wa Marekani.
Donald Trump amependekeza kupigwa
marufuku Waislam kuingia nchini Marekani, pendekezo ambalo
limeshutumiwa mno duniani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni