Kwa mara nyingine uvumi umeibuka kuwa mwanamuziki mahiri na mke wa Jay Z, mwanadada Beyonce ni mjamzito.
Safari hii tetesi hizo zimeibuka baada ya Beyonce kuonekana akiwa amevaa gauni jeusi na juu yake katupia koti eti ili kuficha tumbo lake lisionekane vyema na watu.
Beyonce alikuwa ameongozana na mumewe Jay Z wakitoka kupata chakula cha usiku jumapili katika mgahawa mmoja.
Tayari wawili hao wana mtoto mmoja wa kike aitwae Blue Ivy ambaye wiki iliyopita alifikisha umri wa miaka minne.
Beyonce akiwa mwenye furaha muda wote huku mumewe Jay Z akimfuata kwa nyuma.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni