Hali ya kutoamini na
kulaumiwa kimataifa imeikuta Korea Kaskazini, iliyodai kufanikiwa
kufanya jaribio la aridhini la bomu la hydrogen.
Iwapo jaribio hilo
litathibitishwa litakuwa ni jaribio la nne la Korea Kaskazini
kufanyika tangu mwaka 2006, katika kujiimarisha kijeshi.
Hata hivyo wataalamu wa
nyuklia wanahoji iwapo kiwango cha mlipuko kilikuwa kikubwa kufikia
uwezo wa bomu H.
Latibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Bw. Ban Ki-moon ameshutumu jaribio hilo na kusema kuwa ni
lisilokubalika na linatishia usalama wa ukanda huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni