Waziri wa Mambo ya
Ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere amekosoa namna polisi wa nchi
hiyo walivyoshughulikia tukio la genge lililowashambulia kingono
wanawake Jijini Cologne usiku wa mwaka mpya.
Thomas amesema kuwa
polisi hawapaswi kufanya kazi namna hiyo, kauli ambayo ameitoa wakati
ikibainika kuwa watuhumiwa watatu wa tukio hilo wamebainika.
Zaidi ya wahanga 100
wamelalamika kushambuliwa na genge hilo la vijana wakiume wapatao 30
nje ya kituo cha reli Jijini Cologne.
Mashuhuda na polisi
wamesema watuhumiwa hao huenda walikuwa wenye asili ya Kiarabu ama
kutoka Afrika ya Kaskazini.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni