Kiongozi hatari wa genge linalohusika na dawa za kulevya Joaquin 'El Chapo' Guzman akiwa mikononi mwa polisi baada ya kukamatwa.
Joaquin 'El Chapo' Guzman akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi
Mfanyabishara hatari wa dawa za kulevya nchini Mexico Joaquin "El Chapo" Guzman hatimaye amekamatwa baada ya kuwa mafichoni kwa miezi sita baada ya kutoroka katika gereza lenye ulinzi mkali alikokuwa akitumika kifungo chake.
El Chapo jina lenye maana ya " mfupi mmoja " Kihispania, alikamatwa na polisi katika hoteli moja akiwa na washirika wake katika mji wa Los Mochis katika jimbo la Sinaloa, Mexico.
Katika tukio la kukamwatwa kwake, washirika wake watano waliuawa na wengine sita wamekatwa baada ya kutokea kurushiana risasi. Pia askari mmoja ameripotiwa kujeruhiwa.
Amerejeshwa katika gereza alilokuwa akitumikia kifungo chake kabla ya kutoroka mwezi wa saba mwaka jana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni