.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 9 Januari 2016

WAZIRI NAPE NNAUYE AKUTANA NA WAYHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI LEO JIJINI DAR


Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo na Wahariri  kutoka vyombo mbalimbali vya habari mapema leo,alipokutana nao na  kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabiri tasnia hiyo,mkutano huo  umefanyika kwenye moja ya ukumbi ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Wakuu wa Idara ya Habari Maelezo  na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mh.Nnape Nnauye akizungumza na Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano uliohusu kujadili mambo mbalimbali zikiwemo changamoto zinazoikabiri tasnia ya habari hapa nchini.Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Habari MAELEZO Bi Zamaradi Kawawa akiwakaribisha Wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kwenye mkutano ulioitishwa na  Waziri Nape kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali yanayoikabiri tasnia  ya habari hapa nchini.Pichani kati ni Waziri Mh.Nape pamoja na  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Absalom Kibanda akitoa muongozo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari (hawapo nchini) kuhusina na mkutano wao ulioitishwa na Waziri Nape kujadili mambo mbalimbali na changamoto zinazoikabiri tasnia hiyo kwa ujumla.

Baadhi ya Wahariri wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo.



Mmoja wa Wahariri Kurwa Kaledia kutoka New Habari Hause akiomba ufafanuzi wa  jambo kwa Mh Waziri Nape huku baadhi ya wahariri wakifuatilia kwa  makini.

Mmoja wa Wahariri Grace Hoka akifafanua jambo kwenye mkutano huo

Baadhi ya Wahariri wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo

Baadhi ya Wahariri juu pichani wakishiriki kuchangia mambo mbalimbali kwenye mkutano huo. 

                                  Mmoja wa Wahariri akifafanua jambo kwenye mkutano huo

Baadhi ya Wadau wakubwa wa habari pia walikuwepo kwenye mkutano huo .PICHA NA MICHUZI JR

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni