Mwanasoka Lionel Messi ametwaa tuzo
ya Fifa ya mwanasoka bora wa dunia huku akiwashinda Cristiano Ronaldo
na Neymar.
Hii ni mara ya tano kwa Messi kutwaa
tuzo hiyo ambayo inajulikana kama Ballon d'Or, ambapo amesema ushindi
huo ni zaidi ya jambo lolote alilowahi kuliwazia kufikia akiwa mtoto.
Messi anayechezea Barcelona alipata
asilimia 41.33 ya kura , Ronaldo wa Real Madrid asilimia 27.76 na
Neymar wa Barcelona asilimia 7.86.
Lionel Messi akipongezwa na mchezaji mwenzake Neymar
Cristiano Ronaldo akimsalimia mpenzi wa Lionel Messi
Hali ya mkao wa presha inapanda presha inashuka kabla ya kutangazwa mchezaji bora
Kuanzia kushoto kwenda kulia ni: Thiago Silva, Luka Modric
Marcelo, Paul Pogba, Sergio Ramos, Neymar, Dani Alves, Lionel Messi,
Andres Iniesta na Cristiano Ronaldo wakiwa katika picha ya pamoja
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni