Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius atakata rufaa dhidi ya hukumu ya kutiwa hatiani kwa kumuua
mpenzi wake mwanamitindo Reeva Steenkamp.
Pistorius alimuua Steenkamp Februari
14 mwaka 2013 baada ya kufyatua risasi nne katika mlango wa choo cha
nyumbani mwake alipokuwa amejifungia mpenzi wake huyo.
Hukumu ya kuuwa bila ya kukusudiwa
ilibatilishwa mwaka jana, na kubadilishwa kuwa hukumu ya mauaji.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni