Mamlaka nchini Marekani zimemkamata
mtu mmoja ambaye anaunga mkono kundi la Dola ya Kiislam (IS) ambaye
anatuhumiwa kupanga shambulizi katika jimbo la New York.
Mtu huyo Emanuel Lutchman, 25,
anayetokea Rochester, amefunguliwa mashtaka ya kupanga kuuwa watu
kwenye hoteli wakati wa usiku wa mwaka mpya.
Bw. Lutchman amewaambia mashushusu
wa FBI kuwa alipanga kufanya mauaji kwa kutumia panga na visu.
FBI wamesema kabla ya kukamatwa
alijirekodi kwa video akiahidi kuwa mtii kwa kiongozi wa IS, Abu Bakr
al-Baghdadi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni