Wachezaji wa Manchester City, Sergio
Aguero, Kelechi Iheanacho pamoja na Kevin De Bruyne wameiwezesha
klabu yao kutinga raundi ya nne ya kombe la FA kwa kuifunga Norwich
mbao 3-0.
Sergio Aguero alikuwa wa kwanza
kuzifumania nyavu katika dakika ya 16, kisha Kelechi kuongeza la pili
baada ya kugongeana vyema na mshambuliaji raia wa Argentina Aguero.
Kevin De Bruyne alihitimisha karamu
ya magoli kwa kumfunga bao la tobo kipa John Ruddy katika dakika ya
78.
Sergio
Aguero akipachika bao la kwanza kwa Manchester City
Kelechi Iheanacho akipachika bao la pili la Manchester City
Nayo Manchester United ilipata
ushindi wa mbinde wa bao 1-0 dhidi ya Sheffield United, kufuatia
mpira wa penati uliopigwa na Wayne Rooney katika dakika ya 93, na
kuiingiza Man U katika raundi ya nne ya kombe la FA.
Wayne Rooney akipachika bao pekee kwa mkwaju wa penati
Baadhi ya matokeo mengine ya Kombe
la FA ni :- Wycombe 1 - 1 Aston Villa, Arsenal 3 - 1 Sunderland,
Birmingham 1 - 2 Bournemouth, Brentford 0 - 1 Walsall, Bury 0 - 0
Bradford, Colchester 2 - 1 Charlton, Doncaster 1 - 2 Stoke,
Eastleigh 1 - 1 Bolton, Everton 2 - 0 Dag & Red, Hartlepool 1 - 2
Derby, Huddersfield 2 - 2 Reading na Hull 1 - 0 Brighton.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni