.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 10 Januari 2016

MUIGIZAJI FILAMU SEAN PENN ALIFANYA MAHOJIANO NA JOAQUIN "EL CHAPO" GUZMAN


Muigizaji filamu wa Hollywood Sean Penn alifanya mahojiano na mkuu wa genge la dawa za kulevya Joaquin "El Chapo" Guzman katika eneo la siri mara tu baada ya kutoroka gerezani.

Mahojiano hayo yalifanyika Oktoba mwaka jana katika eneo la jangwa nchini Mexico, yamechapishwa kwenye jarida la jumamosi la Rolling Stone.

Guzman alitoroka kwenye gereza lenye ulinzi mkali mwezi Julai mwaka jana alikamatwa tena Ijumaa na kurejeshwa gerezani.

Mwanasheria Mkuu wa Mexico amesema wameanza hatua zakufanikisha Guzman ambaye hii ni mara yake ya pili kutoroka gerezani, ahamishiwe katika magereza nchini Marekani.
                                                   Joaquin "El Chapo" Guzman akiwa chini ya ulinzi
                  Joaquin "El Chapo" Guzman akipandishwa kwenye ndege baada ya kudakwa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni