Mtanzania Mbwana Samatta
amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika wa mwaka 2015 kwa wachezaji
wa ndani ya Afrika na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) na
kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza kabisa.
Kwa upande wa mchezaji bora wa
Afrika anayecheza nje ya Afrika mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick
Aubameyang amemshinda kwa kura chache Yaya Toure wa Ivory Coast na
kushinda mchezaji bora wa mwaka.
Katika upigaji kura uliofanywa na
makocha na wakurugenzi wa ufundi wa nchi wanachama wa CAF,
Aubameyang alipata pointi 143 na kiungo wa Manchester City, Toure,
akipata pointi 136.
Samatta na Aubameyang, wanakuwa
wachezaji wa kwanza kutoka mataifa yao kuwahi kupata tuzo hizo kubwa
barani Afrika.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni