Nyumba zipatazo 95 zimeteketezwa na
moto baada ya moto wa msitu kuwaka katika mji wa magharibi mwa
Australia.
Watu watatu hawajapatikana huku
theluthi moja ya mji wa kihistoria wa Yarloop, kusini mwa Perth,
umeteketea kwa moto kwa mujibu wa mamlaka za mji huo.
Upepo mkali unaofikia kasi ya
kilomita siti kwa saa usiku wa jana umechochea moto huo wa msituni
uliopachikwa jina la Waroona kiasi cha miale yake kufikia urefu wa
mita 50.
Moto huo bado ni tishio kwa miji
kadhaa na upepo mkali unatarajiwa hii leo ambao utafanya hali kuwa
ngumu zaidi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni