Madaktari wa hospitali ya Taifa ya
Kenyatta Jijini Nairobi jana usiku walikabiliana na kibarua kigumu
cha kuokoa maisha ya mwanamke ambaye alijeruhiwa vibaya kwa kisu
katika ugomvi wa kifamilia uliotokea katika mji wa Wajir.
Bi. Fatuma Ibrahim, 32, alipata
majeruhi ya paja, tumbo na mkono hata hivyo jeraha baya zaidi
lilikuwa la kisu ambacho kimekwama kwenye fuvu la kichwa na madaktari
wa hospitali ya rufaa ya Wajir walishindwa kukitoa na kumuhamishia
hospitali ya Kenyatta.
Dk. Mohammed Hussein, akiongea na
gazeti moja la huko Kenya amesema Bi. Fatuma alipokelewa hospitali ya
Wajir juzi saa nane usiku akiwa na kisu kilichomchoma eneo la kushoto
la uso wake baada ya kutokea ugomvi baiana yake na mwanaume.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni