Mwalimu wa madrasa nchini Kenya
amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kutiwa hadiani na
mahakama kwa kuwafundisha itikadi kali wanafunzi wake katika kaundi
ya Kilifi, Momabsa.
Mwalimu Samuel Wanjala Wabwile
maarufu kama Salim Mohamed, hata hivyo hakupatikana na hatia ya
mashtaka mawili kuwashawishia wanafunzi sita wa shule ya msingi
kujiunga na kundi la Al Shabaab na kuwa wanachama wa kundi hilo.
Katika hukumu hiyo, Hakimu wa
Mahakama ya Mombasa Diana Mochache amesema anaamini kuwa mshtakiwa
alitumia udhaifu wa akili ya kitoto ya watoto hao katika
kuwabadilisha na kuwa na itikadi kali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni