Polisi nchini Ufaransa imempiga
risasi na kufa mwanaume mmoja aliyejaribu kushambulia kituo cha
polisi katika siku ya kumbukumbu ya mashambulizi ya ofisi za jarida
la Charlie Hebdo.
Mtuhumiwa huyo aliyebeba kisu
kikubwa cha kukatia nyama akiwa amevalia vesti bandia ya kujitoa
mhanga ametambulika kama mwizi mzoefu, Sallah Ali, aliyezaliwa
Morocco.
Dakika chache kabla ya kupigwa
risasi mtu huyo, rais Francois Hollande aliwapongeza polisi katika
hotuba yake kwa namna walivyofanya kazi katika tukio la mauaji ya
mwaka jana.
Watu wenye silaha waliuwa watu 17
katika mashambulizi ya mwaka jana wakiwemo wafanayakazi wa jarida la
vikaragosi la Charlie Hebdo na kwenye duka la bidhaa la Wayahudi.
Polisi wakimuangalia mtu aliyeanguka chini baada ya kupigwa riasisi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni